Athari za Kulala Mchana kwa Binadamu



Imebainika kuwa kulala zaidi ya masaa 9 usiku na zaidi ya dakika 90 wakati wa mchana kunaweza kuongeza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi, ”Stroke”

Matokeo haya yameonyeshwa kwenye jarida la “Neurology” lililochapishwa nchini China baada ya kuwafanyia utafiti watu 31,750 wenye umri wa takriban miaka 62.

Mwanzoni mwa utafiti, iligundulika kuwa wale ambao hawakuwa na tatizo la au shida zingine kubwa za kiafya ni wale wanaolala chini ya masaa nane ukilinganisha na wale ambao hulala masaa tisa.
Hatari ya kupooza imeonekana kuongezeka  kwa asilimia 25 kwa watu ambao walipumzika kwa zaidi ya dakika 90 mchana mara kwa mara, ikilinganishwa na wale ambao walipumzika kwa saa isiyozidi moja au ambao hawakulala usiku.
Utafiti pia umebaini kuwa wale ambao hulala kwa muda mrefu usiku na kulala muda mrefu wakati wa mchana wana uwezekano wa 85% ya kupooza.

Wakati wa utafiti huo, watu walichunguzwa kwa muda wa miaka sita na 1557 kati yao walipooza kwenye harakati za kuchunguzwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad