Baada ya Misukosuko Mtume Mwamposa aje Kivingine Atangaza Upako wa KEKI Badala ya Mafuta


Mtume Bonifance Mwamposa amekuja kivingine na kutangaza leo ni upako wa kula keki badala ya kukanyaga mafuta.

Mtume huyo ambaye ni maarufa kwa mafuta ya upako amekuja na staili nyingine ya ulaji wa keki ya upako.

Mara nyingi imezoeleka katika ibada zake ni kukanyaga mafuta ya upako.

Katika tangazo lake lenye kichwa cha habari Inuka Uangaze likieleza kongamano kubwa la kula keki ya upako litakalifanyika leo Februari 16, 2020.

Upako wa ulaji wa keki utafanyika kwa awamu mbili kuanzia saa 2 mpaka 6 mchana.

Awamu ya pili kuanzia saa 7 mchana hada saa 12 jioni katika eneo la Tanganyika packers Kawe jijini Dar es Salaam..


Mtume Mwamposa ambaye anatuhumiwa katika kesi ya vifo 20 vilivyotokea katika ibada aliyokuwa anaiongoza mkoani Kilimanjaro.

Katika ibada hiyo wakati wa kukanyaga mafuta watu 20 walifariki katika kugombea kukanyaga mafuta na kujikuta wakikanyagana.

Katika tukio hilo walijeruhiliwa watu 16.

Baada ya kutokea tukio hilo walikamatwa watu nane akiwemo na Mwamposa kwa ajili ya mahojiano na walipatiwa dhamana.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad