Baadhi ya Mambo Yatakayokufanya Uwe DEREVA Mzuri Zaidi Barabarani


Acha kutumia simu, kugeuka geuka nyuma au maongezi na abiria wako wakati unaendesha. Usisogelee sana gari la mbele yako kwani dharura inaweza kumpata akafunga breki za ghafla au kupasukiwa tairi, akakufanya na wewe uliye karibu kupata ajali

Epuka breki za ghafla. Iwapo utashika kwa ghafla, kuna uwezekano gari ya nyuma ikaleta ajali. Muhimu kukadiria barabara ili ushike breki

Usikae upande uwapo kwenye usukani. Kukaa upande kwenye gari kunaweza kukusahaulisha na kukanyaga mafuta badala ya breki au vinginevyo

Unatakiwa kuwa mvumilivu kwenye uzembe unaofanywa na madereva wengine. Ukiruhusu hasira ikutawale unaweza kujikuta unafanya mambo ya ajabu na ukapata matatizo barabarani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad