Baba Levo: Rayvanny Amenibeba



MSANII kutoka kiwanda cha Bongo Fleva, Clayton Chiponda ‘Baba Levo’ amemwaga shukrani kwa msanii toka pande za Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na kusema kuwa ndiye msanii aliyemrudisha kwenye gemu baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

 

Msanii huyo ambaye pia ni Diwani wa Mwanga Kaskazini, Kigoma Ujiji, amesema kuwa Rayvanny amejitoa sana kukamilisha na kuifanyia promo ngoma ya Zipo aliyomshirikisha Rayvanny na kwa kiasi kikubwa imelirudisha jina lake kwenye ramani.


“Rayvanny ndiye anayenifanya mimi nitoke upya haswa kupitia wimbo wa Zipo kwa sababu aliniahidi atausukuma na amefanya hivyo kweli. Nimemchagua yeye kwa sababu naona tunapatana sana na ikiwezekana ninaweza nikafanya naye ngoma nyingine kama mbili tatu hivi,” alisema Baba Levo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad