JE, Wajua Asili ya NENO Msela na Baharia Kutumika Mtaani?



Inadaiwa Msela ilitokana na neno, ‘Sailor’ mfanyakazi wa meli ambaye sio ofisa au baharia wa kawaida. Huyu ni mtu ambaye alikuwa anasafiri sana na meli kipindi hicho. Waliokuwa wanasafiri wakaita m-sailor, neno hilo likaja kuwa Msela

Miaka ya nyuma watu walikuwa wakijiita ‘masela’ kutokana na kuwaiga watu waliokuwa wamepanda meli na kwenda Ulaya

Walikuwa wakirudi Tanzania wanakuja na vitu vya thamani. Pia walipenda kuninginiza cheni na miondoko yao ilikuwa ni kudunda kutokana na kuishi kwenye meli ambapo muda mwingi walikuwa wakivaa viatu vikubwa na ile hali ya chombo kuyumba kutokana na wimbi

Kipindi cha sasa vijana wengi wanajiita "Baharia" hii ni kutokana na mabaharia kuwa watu wa kusafiri kila eneo, kusaidiana, kuweka kambi popote na kuwa na mahusiano ya kimapenzi kila sehemu atayofika, walikuwa wakitumia msemo wa "New Port, New Wife"

Hii imepelekea sasa vijana wengi mtaani na kwenye kada mbalimbali kutumia neno la baharia au kujiita baharia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad