Balozi Kairuki "Hakuna Mtanzania Aliye China Ameambukizwa Corona"


Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amesema hakuna Mtanzania aliyeambukizwa virusi vya Corona. Anawasiliana na wanafunzi hao pamoja na Serikali ya China ili kufahamu na kutatua changamoto zinazowakabili

Amesema kuishi kwa kufuata maelekezo ndilo jambo linalomfanya hata yeye kubaki hai. Amesema hawaruhusiwi hata kutoka nje na kwamba kitendo cha kukusanyika walichokifanya vijana waliosambaza video siku za hivi karibuni ni hatari sana kwa afya zao

Kuhusu ombi la vijana hao kurejeshwa Tanzania, Balozi Kairuki amesema hakuna usafiri wowote unaoruhusiwa kutoka ama kuingia kwenye mji wa Wuhan na kwamba Japan ilijaribu kuwaokoa vijana wake lakini wakaambukizwa virusi hivyo nchini kwao

SOMA HABARI HIZI KIRAHISI KUPITIA APP YETU YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD HAPA

Amesema Virusi hivyo ni hatari na Serikali ya Tanzania haitafanya kitendo chochote kitakachokuja kuwadhuru Watanzania walio wengi. Kitendo walichokifanya vijana hao kimetokana na msongo wa mawazo unaotokana na kukaa ndani ya uzio wa makazi yao bila ruksa ya kutoka nje

Balozi Kairuki ametoa wito kwa Watanzania kuwaombea Watanzania wanaoishi China ili Mungu awavushe salama na kadhia hiyo. Pia amewaomba wazazi kuwapa faraja vijana wao waliopo China ili waondokane na msongo wa mawazo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad