Bangi ya Kishimba’ Yazua Balaa Bungeni




KWA mara nyingine, Jumanne Kishimba, Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), amesisitiza umuhimu wa kilimo cha bangi na kushauri serikali iruhusu zao hilo. Akizungumza bungeni leo tarehe 3 Februari 2020, mbunge huyo ameelekeza maombi yake kwa George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani.

Si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kutaka kilimo cha bangi kiruhusiwe, tarehe 20 Mei 2019 alisimama bungeni na kuishauri serikali kuruhusu kilimo hicho, kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za binadamu.

Amesema, kilimo hicho kimekuwa na faida kubwa na kwamba, wakulima wa zao hilo wanajificha kutokana na kutokuwa halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kutokana na hali hiyo, ameishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuruhusu kilimo hicho ili kuongeza mapato ya nchi.

Kutokana na ombi hilo, Job Ndugai ambaye ni Spika wa Bunge, ameitaka serikali kuangalia jambo hilo kwa upana kutokana na faida zake. Amesema, nchi ya Canada imekuwa ikipata fedha nyingi kupitia kilimo cha bangi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad