Barwany arusha dongo kwa wanaorejea CCM



Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Lindi mjini( 2010 -2015), Salum Barwany amesema makada wanaorejea Chama Cha Mapinduzi(CCM) kutoka vyama vya upinzani ni wasaka madaraka kwa njia za mkato. Hatahivyo hawawaelezi wananchi sababu sahihi  zinazo wafanya warudi CCM.

Barwany ambae ni makamo mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kanda ya Kusini ameyasema hayo, leo mjini Lindi alipozungumza na Muungwana Blog. Nibaada ya kuombwa atoe maoni yake kuhusu makada wa chama hicho kuendelea kutimkia CCM.

Barwany alisema viongozi wengi walitoka na kurejea CCM ni wale waliojiunga na vyama vya upinzani baada ya kukosa madaraka ndani ya CCM au kushindwa kuteuliwa kugombea uongozi wà umma kupitia chama hicho tawala. Kwahiyo haishangazi kuona wanarejea walikotoka baada ya kushindwa kupata walichotarajia kupata kupitia vyama vya upinzani.

Alisema ni vigumu kwa mwanasiasa ambaye ameanza harakati za kutaka mabadiliko kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini kurejea CCM. Bali ni wale ambao walitegemea na kuvifanya vyama upinzani kama madaraja ya kuvukia na kufikia kile walichokosa wakiwa CCM.

Alisema ni vigumu kwa vigogo waliotoka CCM kuendelea kuhimili misukosuko inayosababishwa na CCM kwa vyama vya upinzani wakati waliyotarajia kupata kupitia upinzani wamekosa na hawana dalili ya kupata kutokanana umaarufu wao kuporomoka.

" Wengine walikosa nafasi ya kugombea Urais,ubunge na udiwani kupitia CCM wakaamua kuja kwetu, nako hawakupata. Kwahiyo hawakuwa na jinsi, bali kurejea walikotoka. Wengine baada ya kupata udiwani na ubunge wameonesha ubora,wakaombwa warudi na kuwahadiwa wataendelea kubaki na nyazifa zao," alisema Barwany.

Alisema wapenda mabadiliko wataendelea kubaki katika vyama vya upinzani. Kwani wao ndio waliosababisha mafanikio na kuvifanya vyama vya upinzani kuaminiwa na kuungwa mkono na wananchi kiasi cha makada wa CCM wenye tamaa ya madaraka kuviona ni kimbilio na daraja la kuwavusha kupata madaraka.

" Lakini kwamakusdi hawataki kuwaambia ukweli wananchi kwanini walikuja upinzani na kwanini wanarudi CCM. Badala yake wanawadanya kwamba walitegemea kwenye upinzani kuna demokrsia, lakini haipo. Demokrasia nikutaka usipigiwe kura kwakuwa uligombea peke yako au upigiwe na kupata kura nyingi kuliko mshindani wako hata kama hukubaliki?," alihoji Barwany.

Kuhusu nguvu ya CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wakati chama hicho kikizidi kukimbiwa na makada wake, alisema hali hiyo inawaimarisha badala ya kuwakatisha tamaa. Kwani wananchi ambao ni wapiga kura wanajua kinachofanyika dhidi ya vyama upinzani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad