Bashe Asema Serikali Imejiandaa kwa Dawa na Ndege Mbili Katika Sakata Nzige

Bashe

Serikali inafuatilia kwa karibu sana suala la nzige wa jangwani. Maofisa na wataalamu wetu wapo katika mikoa ya kaskazini ambako tumepakana na ndugu zetu wa Kenya. Pamoja na hilo tunashirikiana kwa karibu na Wizara ya Kilimo ya Kenya kujua kinachoendelea.

Tumejiandaa kwa dawa na Ndege. Mpaka sasa tuna ndege mbili ktk hatua hii ya awali. Wataalamu wetu wapo wilaya zote za mipakani kutoa elimu na kufanya uchunguzi kwa taarifa yoyote tunayopata hasa pale wananchi wanapotoa taarifa yoyote ile

SOMA HABARI HIZI KIRAHISI KUPITIA APP YETU YA UDAKU SPECIAL 

Hatuwezi ku-undermine threat hii. Hili ni tishio ambalo linapewa uzito stahili. Uelekeo wa upepo umetusaidia lakini taarifa zilizotolewa kuhusu Mkoa wa Kilimanjaro zinafuatiliwa kwa karibu na wataalamu Wizara ya Kilimo kwa siku zaidi ya 14 wapo field tuombe Allah- Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad