Bidhaa kutoka Kenya zakamatwa, Kuteketezwa na kugawiwa kwa watu


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kilimanjaro, Tani 4.5 za majani ya chai, ambayo yanadaiwa kutumika kutengeneza pombe kali za kienyeji.

Bidhaa nyingine zilizokamatwa ni mafuta ya kula Lita 9,482, mfuko mbadala iliyo chini ya viwango tani 7,Sukari tani 4.5, Maziwa ya Bruckside lita 186 na vyombo vya usafiri vilivyotumika kusafirisha bidhaa hizo ambavyo ni Magari Nane, Pikipiki 11 na baiskeli moja.

Akitoa taarifa hiyo leo Februari 13,2019, Meneja msaidizi wa Forodha, Edwin Iwato, amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika kipindi cha mwezi Julai 2019 hadi sasa.

Amesema katika bidhaa hizo, yapo majani ya chai ambayo hutumika kama malighafi ya kutengeneza pombe kali ambazo hutengenezwa kinyemela na kuuzwa jambo ambalo linahatarisha afya za walaji.

“Katika bidhaa za magendo tulizokamata, kwenye doria zetu, Zipo tani 4.5 za majani ya Chai, ambayo yanatumika kama malighafi za kutengeneza pombe haramu, ambapo huyatumia kutia rangi kwenye spiriti na kutengeneza hizo pombe kali za viwandani, jambo ambalo ni hatari kwa afya, “amesema Iwato.

Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi, amesema bidhaa zote zilizokamatwa zina thamani ya zaidi ya Sh239.9 milioni na kwamba zote zinatoka nchi jirani ya Kenya kwa kupitia njia za panya.

“Zipo bidhaa ambazo zitateketezwa ikiwemo zile zilizoisha muda wake wa matumizi, zile ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu na mifuko mbadala ambayo iko chini ya kiwango, lakini zingine zitapigwa mnada na nyingine zitagawanywa kwa wahitaji ili kuepusha kuingia sokoni,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad