"Billnass na Maua Sama Pamechimbika" - Mwana Fa


Mkongwe na mkali wa HipHop hapa nchini Mwana FA, amesema hana uwezo wa kuwasaidia kwa kuwapa sapoti wasanii wote kama ilivyotokea kwa Billnass na Maua Sama, ila kama nafasi ikitokea atawasaidia wengineo ambao watajitokeza.

HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Akizungumza kwenye show ya eNewz inayoruka kupitia East Africa TV kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 12:00 mpaka 12:30 jioni, Mwana Fa amesema ameshawasaidia wasanii wengine kama Maua Sama na Billnass hadi pakachimbika kwa sababu haikuwa rahisi.

"Nimemshika  mkono  Billnass  pia kwa hiyo siwezi kusaidia wasanii  wote kwa wakati mmoja hiyo ni kazi kubwa sana hata kwa Maua Sama penyewe pamechimbika kwelikweli, sisemi kama nimefunga milango, ila kama nafasi ikitokea nikiona kuna uwezekano wa mimi kufanya hivyo nitaendelea kutoa sapoti" ameeleza Mwana FA.

Mengine zaidi aliyozungumza tazama zaidi kwenye video hapo chini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad