BREAKING: Kinana, Makamba Waitikia Wito Wa Kuhojiwa Na Kamati ya Maadili ya CCM


(Pichani) Ndg. Abdulrahman Kinana akiwa ofisini kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula baada ya kuitikia wito wa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili ya CCM.

 *************
Makatibu Wakuu Wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Yusuf Makamba na Ndg. Abdulrahaman Kinana leo Februari 10, 2020 wamefika katika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili inayoongozwa na Ndg. Philip Mangula.

Makatibu Wakuu hao Ndg. Abdulrahman Kinana na Ndg. Yusuf Makamba wamefika katika Ofisi hizo majira ya mchana na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa.

Imetolewa na,
HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad