BREAKING News: Tanzania Yapigwa Marufuku Bahati Nasibu ya viza Marekani

Serikali ya Marekani imepiga marufuku raia wa Tanzania kushiriki katika bahati nasibu wa kupata viza ya kuingia Marekani.

Hatua hiyo inakuja saa chache baada ya serikali ya Trump kumpiga marufuku mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingia nchini humo.

Bahati nasibu hiyo hutoa viza kwa watu takribani 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani.

Nchi ya Sudani pia raia wake wamepigwa marufuku kuingia katika bahati nasibu hiyo.

Wakati huo huo raia wa nchi nne ikiwemo mbili za Afrika Nigeria na Eritrea wamepigwa marufuku kabisa kuomba viza za kuhamia Marekani.

Marufuku hiyo pia itazihusisha nchi za Myanmar na Kyryzstan.

Hata hivyo raia wa nchi hizo ambao watataka kuingia Marekani kwa kutalii ama biashara wataruhusiwa.

Wiki iliyopita, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti juu ya rasimu ya marufuku mpya ya kuingia Marekani kwa mataifa saba.

Ni taifa moja tu la Belarus ambalo lilitajwa katika rasimu ya awali ambalo halijaorodheshwa katika taarifa za leo.


Afisa wa ngazi ya juu nchini Marekani amesema kuwa nchi hizo sita zimeshindwa kufikia "kiwango stahiki cha ulinzi na kupashana taarifa".


"Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbali mwali zimefeli kufikia viwango vya chini tulivyoviweka," Naibu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Chad Wolf amewaambia wanahabari siku ya Ijumaa.

Marufuku ya kwanza ya mwaka 2017 ilikumbana na upinzani mkali ndani na nje ya Marekani.

Bwana Wolf amesema maafisa wa Marekani watakuwa tayari kushirikiana na nchi hizo sita ili kuimarisha matakwa ya ulinzi kwa nchi hizo ili iwasaidie kutoka kwenye listi hiyo.

Nchi hizo mpya zinaungana na nchi nyengine saba ambazo raia wake wamepigwa marufuku kuingia Marekani toka mwaka 2017.

Nchi hizo, nyingi zikiwa na raia wengi Waislamu ni Libya, Iran, Somalia, Syria, Yemen.

Aidha nchi za Korea Kaskazini na Venezuela pia zimo kwenye marufuku hiyo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad