Breaking News: Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye Arejea CCM


Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye leo Februari 10, 2020 ametangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM)

Disemba 4, 2019 alitangaza kuachana na CHADEMA huku akidai alikosea kudhani kuna demokrasia ndani ya chama hicho.

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alijtoa CCM mwaka 2015 ambapo alitangaza rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kuungana Waziri Mkuu wa awamu ya nne, Edward lowassa.

Sumaye alisema kuwa alifikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na uvunjaji wa kanuni ikiwemo katika harakati za kumteua mgombea wa Urais kwa upande wa CCM akidai mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete alitumia ubabe katika kuwaingiza watu wake "tano bora"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad