Bunge la Ulaya Kutumia Simu Kwenye Mikutano yake Kufuatia Virusi vya Corona



Bunge la Ulaya linazingatia kuhusu iwapo linaweza kufanya mikutano na vikao vyake vya awali kwa njia ya simu badala ya kukutana kutokana na kuongezeka kwa wasiwasi kuhusu maradhi ya virusi vya Corona yanayosambaa kwa kasi.

 Msemaji wa bunge hilo amesema wanaliangazia kwa kina suala hilo na kuahidi kutoa ufafanuzi kamili siku chache zijazo.

 Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema, hakuna nchini inayopaswa kudhani kwamba haitaathiriwa na virusi hivyo vya Corona, katika wakati ambapo serikali kuanzia Iran hadi Australia zikipambana kuhakikisha wanafanikwia kuzuia kusambaa zaidi kwa janga hilo linalosambaa kwa kasi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad