Bwana Harusi Achezea Kichapo Siku ya ndoa yake



Bwana harusi alitimuliwa katika harusi yake na umati wa watu uliokua na jazba -baada ya mke wake wa kwanza kuwasili harusini kumfahamisha Bibiharusi kuwa mume anayemuoa alikua ameoa zaidi ya mke mmoja na kwamba ana wake wawili.

Asif Rafiq Siddiqi, ambaye alielezewa kama mwanaume mwenye ndevu mnene wa miaka zaidi ya 30, alisukumwa na kuzabwa makofi na umati wa watu hadi shati yake ilichanika wakati wa ghasia hizo baada ya kufichuliwa kuwa alikua ana wake wawili.

Bwanaharusi alilazimika kujificha chini ya basi na baadae kuokolewa na watu wasi wasiojulikana.

Kuoa mke zaidi ya mmoja inakubalika kisheria nchini Pakistan.

Hata hivyo licha ya kwamba mwanamume anaweza kuoa hadi wake wanne, ni lazima apate idhini ya wake zake wa kwanza kabla ya kuoa tena.

Ilibainika kuwa Bwana Siddiqi alishindwa kutimiza hilo, na Bibiharusi na familia yake walifahamu juu ya ndoa zake za awali pale mke wa kwanza alipoingia kwenye ukumbi wa harusi iliyokua ikifanyika katika mji wa mwambao wa Karachi ambako sherehe zilikua zimepamba moto.

" Kuna tatizo gani dada?" mmoja wa ndugu wa bibiharusi alisikika akiuliza katika video ya tukio hilo liliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanamke , Madiha Siddiqi, hakupoteza muda wa kuelezea kilichomleta ukumbini.

"Ni mume wangu, ni baba wa mtoto huyu. Aliniambia anakwenda Hyderabad kwa siku tatu," alisema mwanamke huyo ambaye alikua amemshikilia mtoto mdogo wa kiume aliyedai ni mtoto wao.

Baada ya hapo familia ilijaribu kumpeleka katika chumba cha pembeni , jambo ambalo lilimpatia fursa ya kuwataja watu ambao alidai walikua ni ndugu zake.

"Yule ni mamamkwe wangu na yule ni jethani [wifi yangu], ambaye alisema kuwa mama yake alikua ni mgonjwa kwa siku tatu na alikua amewekewa drip ," BIi Siddqi alielekea moja kwa moja hadi kwa Bibiharusi (mke mpya) na kumweleza kuwa asifikiri yeyey ni mke wa kwanza

"Hukujua kuwa alikua ni mme wangu? Hata hakufikiria juu ya mtoto huyo ambaye hana hatia."

hata hivyo, haikuishia hapo: Bi Siddiqi alisema kuwa aliolewa na Bwanaharusi mwaka, baada ya kukutana nae katika Chuo kikuu cha Federal Urdu University, ambako Bwana Siddiqi anafanyia kazi.

Halafu akafichua kuwa alioa mke wa pili kwa siri, anayeitwa Zehra Ashraf, ambaye ni mwalimu katika Chuo Kikuu cha Wanawake cha Jinnah kilichopo mjini Karachi, mnamo mwaka 2018.

Kwanza Bi Siddiqi alijua juu ya ndoa hiyo na aligundua kupitia ujumbe ambao aliupata kutoka kwa mke mpya wa mumewe. Siddiqi alisema kuwa Bwana Siddiqi awali alikana kuwa ana mke mpya, lakini baadae alikiri alikua amemuoa mke wa pili.

Ilikua ni Bi Ashraf ambaye pia alimfahamisha Bi Siddiqi kuhusu harusi ya hivi karibuni.

Haijawa wazi ni nini kilichotokea baadae. Hata hivyo polisi walioitwa kwenye eneo hilo wameiambia BBC kwamba ndugu wa Bibiharusi walimvamia na kumpiga Asif, wakachana ngua zake na kumpiga kipigo cha kila aina.


Maafisa walimuokoa Bwana Saddiqi, na kumpeleka kwenye kituo cha polisi cha karibu-lakini ndugu wa Bibiharusi walimfuata na kumsubiri ajitokeze.

Alipotokea tena walimvamia na kumlazimisha kukimbilia chini ya basi. Katika video ya tukio hilo, sauti zilisikika zikimtishia ''atoke chini ya basi au walichome''.

Kwa uoga , aliwajibu kwa sauti ya juu akisema "subirini dakika moja, dakika moja ", huku akisubiri kutambaa kutoka chini ya basi. Alipotoka baadhi ya watu waliingilia kati kuzuwia ghasia.

BBC ilijaribu kuwasiliana na Bwana Siddiqi na ndugu wa mke wake pya kupata kauli zao, lakini hawakupatikana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad