CCM Watoa Kauli Kuhusu Mjadala wa Maridhiano unaozungumziwa na Vyama vya Upinzani



Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi wa CCM Taifa, Ndg. Humphrey Polepole katika mkutano wa Kuadhimisha miaka 43 ya CCM wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, ameeleza kuwa Wamefuatilia mijadala na mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya Upinzani kuhusu kufanya maridhiano, Ndg Polepole anaeleza maridhiano ni hatua na vyama vya upinzani nchini vimeshindwa tangu mwanzo na hata sasa kuzingatia hatua za msingi na za awali kabla ya kufikia hatua ya maridhiano na hivyo kukosa uhalali wa kutaka maridhiano, kwani maridhiano huanza kwa kuwa na uelewa wa pamoja katika mambo ya msingi, pili kujenga muafaka na tatu kuwa  na maridhiano yenyewe.

Akifafanua kuhusu dhana na nadharia ya maridhiano, Ndg. Polepole amesema, kwanza kuwepo na uelewa wa pamoja juu nini watanzania wanataka, kazi kubwa ya maendeleo ambayo imekwisha kufanyika nchini na kubadilisha kabisa hali na ustawi wa watu, pili ni kuwa muafaka wa kitaifa kwa maana ya kukubaliana katika kazi nzuri ambayo imefanyika na katika yale ambayo hakuna muafaka ndio tunakwenda katika maridhiano.

Awali akihutubia mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 43 ya CCM, Ndg Polepole ameeleza ni kwa namna gani Chama cha Mapinduzi kimejipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020, huku akiangazia mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka 43 ya CCM na kwa umahsusi mafanikio ya serikali ya awamu tano chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.

Kauli mbiu ya Miaka 43 ya CCM ni Tuliahidi, Tumetekeleza na Tunaahidi Tena kuchapa kazi kwa juhudi, Ubunifu na Maarifa Zaidi

Imetolewa na;
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad