Breaking News: Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe Ajivua Uanachama wa CHADEMA na Kujiunga CCM


'Kuanzia leo Februari 15, 2020 ninajivua Ubunge wangu na nafasi zote za uongozi ndani ya CHADEMA, na nimeamua kujiunga na CCM' - Cecil Mwambe aliyekuwa Mbunge wa Ndanda.

Katika Uchaguzi mkuu uliofanyika 2015,Cecil Mwambe akiiwakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215.

7 Oktoba 2019 akiwa Mtwara, Cecil Mwambe alitangaza kuwania uenyekiti wa CHADEMA taifa. 19 Desemba 2019 Matokeo yalipotangazwa, Bwana Cecil Mwambe alipata Kura 59 sawa na asilimia 6.2, huku Mshindani wake Freeman Aikael Mbowe akipata kura 886, sawa na asilimia 93.5.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad