China kuanza majaribio ya chanjo ya Corona



Afisa mmoja amesema huenda China ikaanza majaribio ya chanjo ya virusi vya corona mnamo mwishoni mwa mwezi Aprili.

Xu Nanping ambaye ni naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China amesema vikosi kadhaa vya watafiti wanafanya utafiti kujaribu mbinu tofauti za kubuni chanjo na chanjo ya kwanza inatarajiwa kuwasilishwa kwa majaribio mnamo mwezi Aprili.

Watafiti wa serikali na kibinafsi kote ulimwenguni wamekuwa wakishughulika kupata matibabu na chanjo ya virusi hivyo vilivyoibuka kwa mara ya kwanza China mwezi Disemba mwaka uliopita.

Zaidi ya watu elfu mbili mia mbili wamefariki dunia na zaidi ya sabini na tano elfu wameambukizwa nchini China.

Watu wengine kumi na mmoja wamefariki nje ya China huku kukiwa na zaidi ya maambukizi elfu moja katika nchi ishirini na tano duniani.

Shirika la Afya Duniani WHO lilisema Jumanne kwamba huenda ikachukua mwaka au zaidi kwa chanjo ya virusi hivyo kupatikana.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad