China Kusafisha Pesa ili Kukabiliana na Maambukizi ya Corona



Benki kuu ya China imesema kuwa itasafisha, kuzitibu na kuziharibu fedha ikiwa kama njia ya kuzuia ueneaji wa #coronavirus

Pia itazitibu fedha zote katika majimbo yaliyoathirika zaidi na #coronavirus na kuziweka kwenye hifadhi maalumu kwa muda wa zaidi ya siku 14 kabla ya kuzirudisha kwenye mzunguko

Pesa zinazotoka kwenye maeneo yenye hatari zaidi kama hospitali na kwenye masoko zitaharibiwa

Tafiti zimeonyesha kuwa, pesa inayotoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine hubeba uchafu

Orodha ya vitu vilivyoonekana kwenye Dola ya Marekani ni pamoja na Vinasaba, Madawa, Bakteria na Virusi kwa tafiti za 2017 za New York
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad