China yasema juhudi za kudhibiti virusi vya corona zinafua dafu



China imetaja leo kupungua kwa maambukizi mapya ya virusi vya corona kuwa ni ushahidi kuwa juhudi zake za kulidhibiti janga hilo zinafanya kazi, lakini idadi hiyo iliongezeka katika mataifa ya nje huku vifo vikiripotiwa Japan na Korea Kusini.

Idadi ya vifo nchini China imefikia watu 2,118 baada ya watu 114 zaidi kufariki, lakini maafisa wa afya wameripoti kupungua kabisa kwa idadi ya visa vipya kwa karibu mwezi mmoja, ikiwa ni pamoja na mkoa wa Hubei ambao ndio ulioathirika zaidi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema katika mkutano maalum kuhusu virusi hivyo na wenzake wa Kusini mashariki mwa Asia mjini Laos kuwa hali inazidi kuimarika katika mjoa wa Hubei na mji wa Wuhan.

Hata hivyo, afisa kutoka timu ya serikali kuu inayokabiliana na janga hilo amesema hali bado ni mbaya kabisa.

Korea Kusini imeripoti kifo cha kwanza nchini humo lakini idadi ya maambukizi imeongezeka karibu maradufu hadi 104. Karibu nusu ya visa hivyo ni kutoka eneo moja la mji wa Daegu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad