Li Wenliang daktari bingwa wa macho katika hospitali ya Wuhan ambaye pia ni daktari wa kwanza kabisa kuripoti mtandaoni kuhusu kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya Corona mnamo Desemba 30 mwaka uliopita amefariki dunia baada ya kushambuliwa na virusi hivyo, vyombo vya habari China vimeripoti.
Dkt. Wenliang (34) alitoa taarifa hiyo kupitia mtandao akiwa mgonjwa mwezi mmoja tuu baada ya kutangaza kuwepo kwa virusi hivyo na tayari alikuwa amewaona wagonjwa wapatao Saba wenye virusi hivyo ambavyo alivifananisha na virusi vya Sars ambavyo vilitikisa dunia 2003.
Licha ya kuwa Kati ya watu nane waliokuwa wanachunguzwa na polisi na mamlaka za usalama nchini China kwa kusambaza propaganda kuhusiana na virusi hivyo hadi sasa watu 560 wamefariki kwa virusi vya Corona huku watu 28,000 wakiwa wameambukizwa virusi hivyo.