Dk 15 Tu, Tanzanite Queens Inaipiga Uganda




KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite Queens’, Bakari Shime amesema watahakikisha wanafunga mabao mawili ndani ya dakika 15 leo dhidi ya Uganda.

 

Tanzanite inatarajia kucheza mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Uganda, mchezo utakaopigwa jijini Kampala, Uganda. Mchezo wa kwanza uliopigwa Dar, Tanzanite ilishinda mabao 2-1.



Shime alisema: “Nimeshazungumza na vijana wangu na tumekubaliana kuwa lazima tupambane kupata mabao mawili ya haraka ndani ya dakika 15 za kwanza.

 

“Tukifanikiwa tutakuwa tumewapa presha Uganda ya kusaka mabao ya kusawazisha, jambo ambalo litafanya wajisahau na sisi kutumia mwanya huo kupata mabao mengi zaidi.”



Tanzanite inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili aweze kufuzu kucheza hatua ya pili ambapo watakutana na mshindi kati ya Senegal na Siere Leone. Michuano ya Kombe la Dunia itafanyika India kati ya mwezi Juni au Julai, mwaka huu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad