Emmanuel Mbasha Aropokwa Kuhusu kumuoa Muna LOVE..."Mnikome Kama Ameolewa Nifanyaje Sasa"



Msanii wa Injili Emmanuel Mbasha, amewajia juu watu ambao wanamuuliza kuhusu hatma ya Muna Love ambaye taarifa zinasema ameolewa na kubadili dini kuwa muislam na video zinamuonyesha akifunga ndoa ya kiislam.


Taarifa hizo za kuolewa na kubadilisha dini zilisambaa zaidi siku ya jana Februari 7,2020  kupitia mitandao ya kijamii, baada ya Muna Love kuomba kupumzika kutumia mtandao wa Instagram kwa muda.

Kwa Upande wa Emmanuel Mbasha amefanunua zaidi juu ya suala hilo na ametaka watu wamkome kumuuliza kwa sababu sio mume wake na anachojua kuwa Muna ni mpambanaji wa Yesu na mfanyabiashara.

"Jamani nawaomba sana naona simu nyingi na message kuhusu kutaka  interview, nasema mimi sio mme wa Muna mnikome kama anaolewa nifanyeje sasa, ninachokujua kuwa Muna ni kamanda wa Yesu, mpambanaji, na mfanyabiashara. Huko ana-shoot filamu yake, msinisumbue  nazima simu imekua kero msinisumbue mpigieni mwenyewe" ameandika Emmanuel Mbasha

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad