England: Wafanyakazi wa Afya kunyoa ndevu kujilinda na Virusi vya Corona



Wafanyakazi wa afya nchini Uingereza sasa wametakiwa kunyoa ndevu zao ili kuruhusu ‘Maski’ kuzuia maambukizi.

Medics in the NHS have been asked to shave their beards

Onyo hilo linatoka katika picha iliotolewa na kituo cha Marekani cha kudhibiti magonjwa CDC, ikionyesha aina ya ndevu zinazoweza kumfanya mtu kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari.

Inadaiwa wingi wa ndevu inaweza kusababisha ‘maski’ kushindwa kuziba vizuri maeneo ya pua na mdomo na hivyo kuwa rahisi kwa mtu kupitisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa Evening Standard, Viongozi wa Southampton University NHS Trust walituma barua pepe kwenda kwa wafanyakazi wote kuhakikisha wanashughulikia hilo.

Zaidi ya watu 82,000 wamegundulika kuwa na Covid-19 duniani wakati Uingereza ikiwa na idadi ya watu 16 huku 2,700 wakiwa wamefariki dunia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad