Fahamu Haya Kuhusu Fimbo ya Mzee Daniel Arap Moi



Fimbo ya Rais wa zamani wa Kenya, Hayati Daniel Arap Moi iliyotengenezwa kwa pembe za ndovu na dhahabu na kupewa jina la ‘Fimbo ya Nyayo’, ilijulikana sana kama ishara ya nguvu, uongozi na mshikamano wa kitaifa

Mzee Moi hakuwahi kutokea katika kazi yoyote ndani na nje ya nchi bila fimbo yake na alipopanda jukwaani, aliitumia kupungia umati wa watu huku Wachambuzi wakisema fimbo hiyo ilikuwa ishara ya nguvu na mamlaka aliyopewa kutoka kwa jamii yake

Mwaka 1981, alikataa kuonekana kwenye hafla ya Malkia huko Australia bila fimbo yake ambayo kwa wakati huo ilikuwa imevunjika

Fimbo ya Nyayo ilijitengenezea alama yake katika historia, na nyimbo za kizalendo ziliimbwa juu yake, ilikuwa maarufu sana kiasi kwamba iliwekwa nyuma ya noti za Ksh. 20 na Ksh. 100, zilizokuwa na picha ya Moi mbele

Fimbo hiyo pia inaaminika kuashiria maono ambayo Moi alikuwa nayo kwa Kenya changa miaka ya 1970 na 1980

Moi si Rais wa kwanza kwa Ukanda wa Afrika Mashariki kutembea na fimbo, itakumbukwa pia Muasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akitembea na fimbo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad