French Montana Akanusha Kupigwa na 50 Cent




IKIWA zimepita siku kadhaa tangu kusambaa kwa tetesi kuwa rapa toka pande za Marekani French Montana kashushiwa makonde ya nguvu na mwenzie 50 cent katika klabu ya E11 Even Night Club huko Miami, rapa huyo ameibuka na kukanusha tetesi hizo. Kupitia video aliyopost katika mtandao wake wa Instagram Montana alikanusha tetesi hizo.

“Usifanye hivyo wewe ni mtu mzima kufanya vitu kama hivyo hukunigusa wala hujawahi nigusa, nilikuona ulivyowasili na ulipoondoka natamani ungenigusa” alisema Montana. Aidha, rapa huyo alienda mbali kwa kudai 50 alihonga ili apatiwe heshima ya nyota kama ilivyo utaratibu maalum wa Hollwood Walk of Fame wiki iliyopita.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad