Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameagiza polisi kuwasaka na kuwachukulia hatua watu waliotumia Mitandao ya amii kuonesha ubovu wa miundombinu ya barabara ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
RC Gambo amesema kitendo hicho ni sawa na uhujumu uchumi kwani watu hao wangeweza kutumia njia sahihi kuwasilisha taarifa hizo na si kutumia mitandao ya kijamii.
RC ARUSHA: WALIOSAMBAZA PICHA KUONYESHA UBOVU WA BARABARA NGORONGORO WAMEHUJUMU UCHUMI
— Jamii Forums (@JamiiForums) February 16, 2020
> Aagiza Polisi kuwasaka, kuwakamata na kuwahoji wahusika
> Asema wanachafua taswira ya nchi kwani kulikuwa na njia sahihi kuliko kutumia mitandao; kitendo alichokifananisha na Uhujumu Uchumi pic.twitter.com/XtSn3hhe52