Kuhusu Mwanamuziki Gelly wa Rhymes Kulelewa na Jimama Arusha


Msanii Gelly Wa Rhymes amefunguka na kusema yeye ni bishoo lakini ni mpambanaji na watu wasimchukulie poa, kama analelewa na mwanamke ambaye amembadilisha dini na kumuhamisha Jiji.

Gelly Wa Rhymes ameeleza hayo alipodakwa na kamera za EATV & EA Radio Digital, ambapo amesema Dar es Salaam ndipo wanaume wanaongoza kulelewa na wanawake ila sio Arusha  anapoishi kwa sasa.

"Watu waniangalie vizuri aisee mimi ni bishoo, nahangaika,  mpambanaji na sikai kizembe, halafu ule Mkoa wa Arusha watu hawaishi hivyo labda huku Dar ndiyo vijana wanalelewa, watu wa kule wamenifundisha maisha ya kukaza maisha yangu ndiyo yapo hivo" amesema Gelly Wa Rhymes.
SOMA HABARI HIZI KIRAHISI KUPITIA APP YETU YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD HAPA

Aidha ameongeza kusema watu watakuwa wanafeli endapo watamchukulia kama mtoto wa mama asiyeweza kazi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad