Godbless LEMA "Kabendera itabidi Aombe Msamaha Kwa Mungu kwa Kukiri Uongo"


Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema Erick Kabendera baada ya kukiri kosa na kuachiwa huru sasa ana wajibu mbele za Mungu.

Amesema wajibu huo ni kuomba msamaha kwa kukiri uongo, hivyo atapaswa kutubu dhambi hiyo na Mungu atamsamehe.

“Ibrahimu alishawahi kumwita Sara mkewe kuwa nk Dada yake ili asiuawe na Mungu akuchukia,” aliandika Lema.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu.

Mashtaka hayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 milioni.

Kwa uamuzi huo sasa Kabendera atakuwa na mashtaka mawili ambayo ni kukwepa kodi na kutakatisha fedha.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Februari 24, 2020 na wakili wa Serikali mkuu, Faraja Nchimbi  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Janeth Mtega wakati akimsomea mashtaka mshtakiwa huyo.

Kabendera amekiri mashtaka yake mawili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad