Good News: Dawa ya Kutibu Virusi vya Corona yapatikana



TELEVISHENI ya taifa ya China imetangaza kuwa dawa ya kutibu wagonjwa walioathiriwa na virusi hatari vya corona imepatikana.

Imetangaza jana kuwa timu moja ya watafiti katika maabara ya Zijianga nchini humo imeweza kutengeneza dawa inayotibu wagonjwa wa kirusi cha corona.

Hata hivyo, televisheni hiyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu habari hiyo.

Huku hayo yakiripotiwa, kamisheni ya taifa ya usalama na afya nchini China jana asubuhi ilitangaza kuwa, hadi hivi sasa watu 492 wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa unaotokana na virusi hatari vya corona na zaidi ya 24,324 wameshaambukizwa virusi hivyo.

Virusi hatari vya corona vilianza kujitokeza kwa mara ya kwanza Disemba mwaka jaan katika mji wa Wuhan, mkoani Hubei nchini China.

Hadi hivi sasa virusi hivyo vimeshaenea katika mikoa zaidi ya 30 ya China na nchi nyingine 18 duniani.

Hii ni katika hali ambayo, Jumapili wiki iliyopita madaktari nchini Thailand walidai kuwa wamefanikiwa kupata dawa ya kutibu ugonjwa wa corona kutokana na kuchanganya dawa za kutibu HIV na influenza.

Madaktari hao walidai kuwa matokeo ya waathiriwa wa virusi vya corona waliotumia mchanganyiko huo ni mazuri.

Kabla ya hapo, pia maofisa wa afya nchini China walikuwa nao wametangaza kwamba wameanza kutumia mchanganyiko wa dawa za kutibu HIV na infuleanza kwa ajili ya wagonjwa wa virusi vya corona na matokeo yamekuwa ya kuridhisha.

Siku ya Jumapili jeshi la China lilikabidhiwa rasmi hospitali ya kwanza ya muda ya kupambana na wimbi la maambukizi ya virusi hatari vya corona katika mji wa Wuhan wa katikati mwa China.

Hospitali hiyo ya muda inayoitwa Huo-Shen-Shan imejengwa kwa muda wa siku tisa tu na ina vitanda 1000. Wagonjwa wa virusi vya corona walianza kupewa huduma za tiba kwenye hospitali hiyo kuanzia leo Jumatatu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad