HAJI Manara Atema Nyongo Asema Hakuna Mchawi Simba Haiwezi Kushinda Mechi zote

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amefunguka kuhusu kufungwa katika mchezo wao wa jana akisema Simba haiwezi kushinda kila siku na kila mechi.

Manara alikuwa akijaribu kuwatuliza mashabiki baada ya kipigo cha bao 1 kwa bila kutoka kwa JKT Tanzania.

Muongeaji huyo maarufu katika soka la Bongo amesema JKT walikuwa bora uwanjani kuliko Simha na walistahili ushindi katika mechi hiyo.

Amesema Simba ni timu kubwa haipaswi kulia lia na kuteteleka kisa kufungwa mchezo mmoja. Muhimu ni kujipanga kwa mechi zijazo.

Amesema hakuna hakuna mchawi na matokeo ya soka ndivyo yalivyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad