Heche Amcharua Kigwangalla Amuuliza Kama Ubovu wa Barabara ni Taarifa nyeti?



Mbunge wa Tarime vijijini (Chadema), John Heche, ametolea povu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla huku akimhoji barabara mbovu ni taarifa nyeti.

“Hivi mbona hata watu wenye akili mnajitoa sana akili kipindi hiki? Dawa ya barabara mbovu irekebishwe,”

Kiongozi huyo aliendelea kuandika kuwa “Hata tour guides wasipotoa wazungu au wageni wenyewe wakipita hapo watashare na kuwaambia wenzao kuhusu ubovu wa barabara,” aliandika Heche.

Jana waziri Kigwangalla alisema watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na kulinda taarifa nyeti za nchi.

“Wenzetu hata wakipigwa mabomu na magaidi huwa hawaweweseki na kulaumiana kwa sababu ya kulinda jina na hadhi ya nchi yao kwa ajili ya biashara sisi tour guides wetu wa naona kuwa hiyo ni fursa ya kulaumu,”.alisema Kigwangalla
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad