Mkunga ni aina ya Poraquê (Electrophorus electricus) anayeweza kuzalisha Volts 650 za umeme na hutumia umeme huo kujikinga dhidi ya maadui zake
Anaweza kukua hadi kufikia urefu wa Mita 1.8 na anaishi kwenye maji baridi na anapenda mazingira ya tope. Wale wanaoishi kwenye maji chumvi maarufu kama Ibrahimu huzalisha Volts220 tu
Samaki huyu ni kiumbe aliyevunja rekodi ya kuzalisha umeme mwingi ambapo pigo lake moja (umeme) linatosha kumfanya mtu akose nguvu na azame majini, akipiga mara tatu ana uwezo wa kuua
Inasemekana kuwa dhana ya kuwa mtu ameliwa na Chunusi inatokea pale Samaki huyu anapompiga shoti mtu na kufanya azame majini na kufa na kwa kuwa samaki hawa huishi kwenye tope, watu wengi wanataja Chunusi hukaa maeneo ya tope