Inakadiriwa kwamba takriban watu milioni 240 duniani huenda mitandaoni kutafuta mpenzi kulingana na Statista, lakini unajua kwamba sio wote wanaofanikiwa kupata mpenzi?
Hivyobasi tumeweka mbinu zitakazokuwezesha kumpata unayemtafuta kwa udi na uvumba kupitia The Man Diet na shangazi Suzie Heyman.
1. Usitafute mpenzi kwa sababu unatafuta tu!
Usijilazimishe iwapo hutakiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption Usijilazimishe iwapo hutaki
Iwapo hutaki acha. Iwapo haumpendi mtu usijaribu kutaka kumuona tena
‘Kujaribu ni hatari – kunatupeleka mbio, na kutufanya kuchoka kutupatia hisia mbaya kuhusu sisi binafsi na wengineo.
2. Jiamini
Iwapo humuamini mchumba wako chukua hatua haraka iwezekanavyo
Iwapo utaona onyo lolote mbele yako chukua tahadhari. Kuna vishawishi vya kufikiria: Ni makosa yangu – pengine ni makosa yao.
Wekundu wa lawaridi
3. Utafiti wa hivi karibuni unasema kwamba ujumbe mchache wa simu ni bora zaidi ya kutuma ujumbe mwingi
Mawasiliano mengi ya bila mpango kwa simu hayafai
Kutumiana ujumbe na watu 100 kwa muda kutakufanya uchoke haraka.
Wekeza muda wako kwa wale wanaopendelea kutumiana ujumbe nawe, wale ambao unadhani wana hisia kama zako.
4. Kuchumbiana ni mchezo wa nambari-nenda kule ambako kuna watu wengi.
Ni vyema kutafuta mchumba mahala penye watu wengi badala ya jangwani
Epuka huduma za kuchumbiana nenda kule ambako kuna watu wengi.
Kuchumbiana ni mchezo unaotegemea nambari hivyobasi kutafuta almasi katika pandashuka unahitaji pandashuka.
Usikubali bishara inayodai kwamba ina almasi ndani ya vitabu. Hawana. hakuna njia fupi .
5.Tafuta marafiki kwanza
Inapokuja katika uhusiano- urafiki ni kiungo muhimu kuanzia
Uhusiano mzuri huonekana unapoanza kuwa marafiki kabla ya kuwa na uhusiano.
Na inawezekana ukapata mpenzi kutoka kwa rafiki yako.
6. Jenga urafiki na kila mtu
Wewe sio tabaka langu – hata wewe pia!
Unaweza kufikiria unajua kile kinachokuvutia lakini…..
Unapopunguza orodha ya marafiki , huenda ukamkosa mtu unayeweza kuelewana naye na ambaye unadhania sie nyonda mkalia ini kwa kumtazama tu.
7. Kuwa mwangalifu na mwenye busara
Kuchumbiana mitandao kunaweza kukuletea furaha – lakini hakuwezi kukuzioa kufanya utafiti ili kufanya uamuzi wenye busara
Hatari moja ya mtandao ni kwamba hamuna mawasiliano hivyobasi hujui chochote kuhusu mutu uliekutana naye. Jieleweshe kwa haraka kuhusu sababu fulani ambazo unadhania hazieleweki.
Ombi lolote la fedha kutoka kwa mchumba wako mpya ama mtu ambaye kila mara anavunja mipango – ni mojawapo ya sababu zinazokwambia uliekutana naye hafai hivyobasi katiza mawasiliano naye.
Usikubali kupatikana katika penzi lisilo na hisia zozote.