Jacqueline Mengi alalamika kufukuzwa kuingia kwenye kaburi la Mengi


Jacqueline Mengi amesema amenyamaza kwa mambo mengi na kwa sasa anazuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wake.

Amesema anafukuzwa kuingia katika kaburi hilo pamoja na watoto wake na kutakiwa kuomba ruhusa ya kuingia katika kaburi hilo.

Jacqueline aliandika ujumbe huo leo katika ukurasa wake wa Twitter huku akisema hatakubali kuendelea kuonewa na watoto wake.

Aliandika ujumbe huo “Nimenyamaza kwa mengi sana tu. Mmefikia hatua ya kunizuia Mimi na wanangu kuingia kwenye kaburi la mume wangu, tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la mume na baba wa watoto wangu!.. Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya,” aliandika Jacqueline.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jakline, USIKUBALI LAZIMA UWE NGA NGARI
    Muie Manyama Funua kesi na Wewe na watoto wa Marehemu hao Wadogo
    wana hali sawa na hao ndugu zao.

    Wacha Sheria ichukuemkondo wake fungua RB LEO LEO .
    Uweze kuijengea kesiyenye Mmashiko. siyo Fesibuku waa twita havi saidii. Pole mdada. Changamka naWakiliwako.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad