Jalada la Kesi ya Aliyekuwa Mchunguzi Mkuu TAKUKURU Bado Lipo kwa DPP



Jalada la kesi ya  aliyekuwa Mchunguzi Mkuu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyita (44) lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Batanyita anakabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kuomba rushwa milioni 200 na kutakatisha fedha katika kesi ya uhujumu uchumi namba 76/2019.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  Februari 7, 2020 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya, amesema kuwa jalada hilo kabla ya kupelekwa kwa DPP lilirudishwa polisi kutokana na baadhi ya maeneo kuhitaji kufanyiwa uchunguzi wa ziada.

Hakimu Isaya baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 21, 2020 itakapotajwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad