Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema yeye aliachia kijiti kwa kina Antonio Nugaz lakini mwenzake Haji Manara bado kakomalia sijui ndio msukule wa Simba.
Amesema ni vizuri kupokezana vijiti ama awaaachie wengine kama vipi arudi akafundishe madrasa.
“Mimi niliachia kijiti kwa kina Antoni Nugaz, lakini upande wa @SimbaSCTTanzania mwenzangu kakomalia hapo sijui yeye ndio msukule wa Simba alaaniwe amtegemeaye mwsnadamu yeye kila muda Moooo… Mooooo,” amesema Jerry
Muro ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Arumeru ameyasema hayo leo ambapo amesema amerudi tena Yanga washirikiane na kwamba kesho wanatarajia ushindi.
“Nimekuja tena Yanga sikuitwa ila karaha na fedheha zimezidi nikaona nije tena tushirikiane,” amesema.
Aliongezea kuwa:” Viongozi wote wa Yanga wenye hela rudini tuishi kama tulivyokuwa tunaishi zamani na mnajua, mwenye gari alete, aliyekuwa anamwaga upupu amwage na aliyekuwa anatoa hela atoe,” amesema Jerry.
'Mimi niliachia kijiti kwa kina Antonio Nugaz, lakini upande wa @SimbaSCTanzania mwenzangu kakomalia hapo hapo sijui yeye ndio msukule wa Simba' - Jerry Muro#YangaPress pic.twitter.com/PdUFxQYTBI— East Africa TV (@eastafricatv) February 25, 2020
'Nimekuja tena Yanga sikuitwa ila karaha na fedheha zimezidi nikaona nije tena tushirikiane' - Jerry Muro#YangaPress pic.twitter.com/tByv6YWl9F— East Africa TV (@eastafricatv) February 25, 2020
'Viongozi wote wa Yanga wenye hela rudini tuishi kama tulivyokuwa tunaishi zamani na mnajua, mwenye gari alete, aliyekuwa anamwaga upupu amwage, aliyekuwa anatoa hela atoe' Jerry Muro#YangaPress pic.twitter.com/zjwObnGBpH— East Africa TV (@eastafricatv) February 25, 2020