Julian: Mwanamke Asiye na Uke Wala Mfuko za Uzazi


Julian Peters mwanamke wa miaka 29 kutoka nchini Kenya aliyezaliwa na ugonjwa unaojulikana kama (MRKH) Mayer-Rokitansky-Küster-Hauser, tatizo ambalo huwaathiri sana wanawake na hasa katika  kizazi cha mwanamke.

Na kwa tafsiri rahisi ni kwamba Julian alizaliwa bila uke na na njia ya uzazi. Bi Julian  anasema hali hii ninayoishi nayo inachangamoto nyingi kwani kila siku anakabiliana na hisia mseto, mbali na hayo jamii inayonizunguka pia wakati mwengine inataswira tofauti kuhusu hali yake.

Julian anasema kuwa maoni ya jamii yanatofautiana kuhusu hali yake kwani kuna wale ambao wanaamini kuwa hali anayoishi nayo sio ugonjwa bali ni jambo aliliojiletea mwenyewe, pengine kwa dhana kuwa aliavya mimba nyingi au pengine aliwahi shiriki maswala ya ushirikina.

Kulingana na daktari Mutindi Kakuti wanawake wenye ugonjwa huu wanaweza kushiriki ngono endapo watafanyiwa upasuaji wa kurekebisha njia au sehemu ya kike.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad