Kiukweli Rais Magufuli ndio mwanasiasa pekee Tanzania aliyeanza moto na anamaliza miaka mitano moto bila kupoa


Moto alioanza nao ndio anamaliza nao. Kuna watu tulidhani pumzi itakata katikati ya safari ila hilo halijaonekana.
Ameanza kwa kuogopwa na anamaliza kwa kuogopwa.

Hili nililithibitisha siku amezushiwa kufariki mitandani, Kuna jamaa mmoja mtumishi wa Umma alishukuru akasema afadhali aondoke tuanze kupiga madili. Basi nikajua kumbe jamaa moto haujakata.

Hadi leo maofisini pakisikia Rais anakuja, kiwango cha hofu kama mtu atimizi wajibu kiko vilevile kama alivyoanza kazi.

Kiukweli tukubali au tukatae Rais Magufuli amekuja na suprise kubwa kwenye siasa na utumishi wa umma. Amefaulu kuanza na kumaliza kama alivyoanza bila kulegea wala kuchoka, wala kukpomromise misimamo yake na style yake ya kuongoza.

Hii imenifundisha kitu, hata katika mambo madogo madogo na viuongozi vyetu huku mitaani. Amenikumbusha yule Mtanzania aliyevunja rekodi ya mbio za masafa marefu kwa kuanza kwa kasi na kumaliza kwa kasi akiongoza huku wengine wakitegemea atakata pumzi njiani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad