Linah Sanga Ajitapa kuwa Mama wa Kishua



MWANAMAMA kunako Bongo Flevani, Esterlina Sanga ‘Linah’ au ‘Ndege Mnana’ amesema, watu wengi wanamwambia kuwa anaonekana kama hana mtoto, lakini ukweli ni kwamba yeye ni mama wa kishua. Linah ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Tracy aliyezaa na dairekta wa filamu za Kibongo, Shaban Mchomvu.

Mwimbaji huyo mwenye sauti matata, ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, anaonekana mdogo au hana mtoto kutokana na namna anavyojiweka na kujitengeneza. “Mimi ni mama wa kishua ndiyo maana wengine hawaamini kama nina mtoto kwa sababu ninajipenda na natamani mtoto wangu naye awe kama mimi,” amesema Linah.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad