Majambazi yapora Karatasi za Chooni kwa Silaha



Wanyang'anyi wenye silaha waliopora maelfu ya karatasi za chooni wanasakwa na polisi wa Hong Kong, jiji lililokumbwa na uhaba wa bidhaa kutoka na na ugonjwa wa homa ya virusi vya corona.
Karatasi za chooni zimekuwa bidhaa adimu katika jiji hilo la biashara, licha ya serikali kuhakikishia wananchi kuwa ugavi wa bidhaa hautaathiriwa na mlipuko wa virusi vya corona.
Maduka makubwa yamejikuta yakishindwa kujaza kwa haraka bidhaa zinazoisha, na hivyo wakati mwingine kusababisha misururu mirefu huku makabati ya kuwekea bidhaa yakigeuka matupu muda mfupi baada ya maduka kufunguiliwa.

Pamoja na karatasi za chooni, kumekuwa pia na uhaba wa vyakula kama mchele na viazi pamoja na karatasi za kusafishia mikono na nyingine za usafi.
Polisi walisema dereva wa lori alizuiwa na watu watatu mapema leo asubuhi akiwa nje ya duka katika eneo la Mong Kok, wilaya wanayoishi watu wa kada ya wafanyakazi na ambalo lina historia ya makundi ya uporaji.

"Mtu anayehusika na usambazaji alitishiwa kisu na watu watatu ambao walichukua karatasi za choono zinazogharimu zaidi ya dola 130 (sawa na Sh360,000)," msemaji w apolisi aliimbia AFP.
Picha za televisheni zinawaonyesha wapelelezi wa polisi wakiwa wamesimama kuzunguka maboksi ya karatasi hizo za choono nje ya supermarket.

Msichana mmoja aliyekuwa akipita eneo hilo alihojiwa na kituo cha televisheni cha iCable alisema: 

 "Ningeiba kikinga uso, lakini si karatasi ya choono."

Jiji hilo, ambalo tayari watu 57 wamegundulika kuwa na virusi hivyo, linakabiliwa na tatizo kubwa la vikinga uso.

Hisia za woga zilizotanda sehemu kubwa ya Hong Kong tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi hivyo vipya vya corona, kwa kiasi fulani zinasababishwa na historia ya jiji hilo ya kukumbana na magonjwa hatari.

Mwaka 2003, watu 299 walipoteza maisha kutokana na mlipuko mwingine wa virusi vinavyosababisha homa ya mapafu, SARS, mlipuko ulioanzia bara nchini China.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad