Makaburi ya Halaiki Yenye Maiti 6000 Yapatikana Burundi....



ZAIDI ya miili 6000 imepatikana katika makaburi ya halaiki nchini Burundi huku maiti 6032 na maelfu ya risasi yamegundulika katika makaburi sita ya halaiki katika eneo la Karusi nchini humo.

Mamlaka nchini Burundi imetangaza kugundua zaidi ya miili 6000 katika makaburi sita ya watu waliozikwa kijumuiya.

Yaliyogunduliwa katika eneo la Karusi ni makubwa kutokea tangu Serikali itangaze kuanza kwa kampeni ya kugundua makaburi hayo mwezi Januari 2014.

Pierre Claver Ndayicariye Mwenyekiti wa Kamisheni ya ukweli na maridhiano ya Burundi amevieleza vyombo vya habari kuwa mabaki 6032 pamoja na maelfu ya risasi yamegundulika na hiyo ni pamoja na nguo, miwani na rozari ambavyo vilitumika kuwagundua baadhi ya wahanga.


Ukirejea mauaji ya 1972 ambayo iliaminika kuwa iliwalenga watu wa kabila la Hutu, Ndayicariye amesema kuwa familia za wahanga ziliweza kuvunja ukimya uliohifadhiwa kwa miaka 48.

Imeeleza kuwa Kamisheni hiyo iliundwa mwaka 2014 kufuatia jinai zilizofanyika mwaka 1885 hadi 2008 na hadi sasa wamegundua makaburi ya halaiki 4000 yenye miili 142,000 ya wahanga wa jinai ya vita.

Idadi hiyo kubwa ya makaburi kuwahi kutokea nchini humo iwewashtua watetezi wa haki za binadamu na kueleza kuwa jinai zizofanywa na Rais Pierre Nkurunzinza zifuatiliwe pia.

Si mara ya kwanza kwa makaburi ya jumuiya kugunduliwa nchini Burundi na Serikali ya Bujumbura pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Burundi yamekuwa yakipinga ripoti za mashirika ya kutetea haki za binadamu kama Amnesty International na Human Rights Watch yanayodai kuwa bado kunashuhudiwa ukandamizaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo.

Machafuko yameendelea kuikumba Burundi tangu mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake cha CNDD-FDD kuwania tena urais kwa mara ya tatu na baadaye chama hicho hivi karibuni kilimteua Katibu Mkuu wa chama hicho, Evariste Ndayishimiye kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika mwezi Mei mwaka huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad