Makete:Wasichana hulazimika kutumia shumizi za wenzao kama Pedi




Baadhi ya wanafunzi wasichana wa shule za sekondari wilayani Makete mkoani Njombe inaelezwa hulazimika kutumia nguo za ndani za wenzao kama pedi kutokana na wakati mwingine kuishiwa fedha za kununua vifaa hivyo wanapokuwa hedhi.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya walimu walezi mara baada ya shule tano katika tarafa za Bulongwa na Magoma wilayani Makete mkoani Njombe wanafunzi Wapatao 920 kupewa msaada wa taulo za kike kutoka kwa wadau wa maendeleo jamii kama njia mojawapo ya kuwapunguzia gharama za manunuzi ya vitu hivyo muhimu.

Walimu wa shule hizo wamesema wapo baadhi ya wasichana kutokana na kukosa fedha za kununulia taulo za kike wanalazimika kuchukua nguo za ndani za wenzao na kuzitumia kama pedi

"Kwanza ambayo kuna watoto wengine walikuwa wanapata,walikuwa wanatumia shumizi utakuta mwenzie kaanika yeye anaiondoa anaitumia kujistili,wakati mwingine unamruhusu aende nyumbani akiludi analudi bila hivi vifaa,watoto wetu wamefurahi sana kupata msaada"alisema mmoja wa wlimu katika shule iliyopata msaada

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Mchungaji Anjelika Sanga ameamua kutoa sehemu ya fedha inayopatikana kutokana na mauzo ya nyimbo zake za injili anazoimba na kushirikiana na wadau wapenda maendeleo ya watoto wa kike na kuamua kununua taulo za kike kwa wasichana wa shule za sekondari wilayani Makete zoezi ambalo amesema litakuwa endelevu,Mchungaji Anjelika amesema kutokana na changamoto nyingi wanazopitia wanafunzi wa kike wanapopata hedhi, imepelekea kuguswa na kutoa msaada huo kwa kuwa wanafunzi hawalingani uwezo

"Nimeamua kutoa taulo kwasababu mara nyingi wanapokuwa kwenye siku zao wanapata shida na wanakosa pia masomo,mwanafunzi mwingine utakuta kwa mwezi anakwenda hedhi siku tatu mpaka nne au tano ukipiga mahesabu kwa siku hizo hajahudhulia masomo utakuta kwa mwezi amepoteza vipindi vingi sana,jamii ijue kuwa hiki ni kitu kipo kwa mwanamke tuwasaidie "alisema Anjelika Sanga

Aidha kakatika zoezi hilo amesema amegundua kuwa wanafunzi wamefurahi na bado wanahitaji kuhudumiwa,hivyo atalazimika kukabidhi msaada huo mara kwa mara katika wilaya hiyo ili kuwapa zaidi furaha watoto wa kike.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule za sekondari zilizonufaika na msaada huo kutoka Usulilo, Kipagalo, Bulongwa, Ipelele na Mwakavuta wameelezea furaha waliyonayo baada ya kugawiwa taulo hizo za kike

"Mimi kama mwakilishi wa wanafunzi wenzangu wa Bulongwa sekondari tunapenda kushukuru kwa msaada wa taulo za kike tunawashukuru sana kwa mchungaji Anjelika na Mungu ambariki"alisema Stela Mayai mwanafunzi wa kidato cha tano mchepuo wa HKL

Awali kabla ya kugawa taulo hizo amewataka wanafunzi hao kuzingatia masomo kwa kuwa wazazi wao wamewekeza kwao hivyo watambue wanategemewa na wazazi na taifa kwa ujumla.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad