Makubwa..Auawa kwa Kuchomwa Mkuki Kisa Mapenzi


Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Hawa Juma (35) mkazi wa Kijiji cha Isikizya wilayani Uyui Mkoa Tabaro ameuawa kwa kuchomwa mkuki mgongoni na mumewe alipokuwa amelala nyumbani kwake.

Uchuguzi wa awali wa polisi unasema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na mtuhumiwa ameshakamatwa na jeshi la polisi mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa,amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo saa nne.

Amesema mtuhumiwa huyo ambaye jina lake ni Omary Kabi,alimchoma mkewe Hawa Juma Seif (35) na mbinu aliyotumia ni kumvizia.

“Kama huyu mwanaume sasa anakabiliwa na kesi na kuiacha familia haina mwangalizi na akifungwa na  familia inabaki inateseka,”amesema Mwakalukwa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad