Manara Awaweka Pamoja Molinga, Bocco, Ally Ally na Wawa, Mashabiki Wafunguka


Haji Manara

Wakati klabu kongwe Simba na Yanga zikijiandaa kuendelea na michezo ya ligu kuu ya Vodacom Tanzanania bara Msemaji wa wanyama wa Msimbazi Haji Manara amewafananisha mshambuliaji Bocco wa Simba na Molinga wa Yanga.

Leo Simba itakabiliana na Mtibwa huku Yanga ikiminyana na Mbeya City michezo ambayo ni muhimu kwa kila timu kupata ushindi.

Wakati yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya mechi hizo manara aliposti video fupi ya mchezo wa soka ikionyesha mshambuliaji akiamua kuacha kufunga na kutoa mpira nje baada ya beki wa timu pinzani aliyekuwa akikimbizana naye kupata shida ya misuli na kusema hiyo ndiyo fair play.

Alisema “Ukisikia Fair Play ndio hii sasa.. Pata Picha Molinga kabaki na Wawa halaf kafanya fair play kama hyo au Bocco kabaki na Kindoki ahh sorry Ally Ally itakuwaje!!!”.
SOMA HABARI HIZI KIRAHISI KUPITIA APP YETU YA UDAKU SPECIAL 

Hata hivyo baada ya posti hiyo mashabiki walitiririka katika ukurasa huo wakitoa tofauti wapo waliomshambili kwa Mwenendo wa Simba wa sasa na kuna walielezea kitendo hicho wakisema kwa soka la bongo hakiwezekani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad