Manchester City yaitandika 2-1 Real Madrid



Club ya Man City ya England safari yake ya kwenda katika jiji la Madrid nchini Hispania kukipiga na club ya Real Madrid katika hatua ya 16 bora imekuwa na manufaa baada ya kufanikiwa kupata ushindi mnono na kuandika historia mpya katika club yao.

Man City wakiwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid kukipiga dhidi Real Madrid katika mchezo wa UEFA Champions League wamefanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 2-1, magoli ya Man City yamefungwa wakitokea nyuma baada ya Isco dakika ya 60 kufunga goli la utangulizi kwa Real Madrid.

Gabriel Jesus ndio alianza harakati za kuikomboa Man City kwa kufunga goli la kusawazisha dakika ya 78 kabla ya dakika ya 82 Kevin De Bruyne kufunga goli la ushindi la Man City kwa mkwaju wa penati, Man City katika game hiyo waliandika historia ya kuifunga Real Madrid kwa mara ya kwanza katika maisha yao, ilimalizika Real Madrid wakiwa pungufu baada ya kuoneshwa kwa kadi nyekundu kwa nahodha wao Sergio Ramos dakika ya 85.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad