Marekani Yaionya KENYA Dhidi ya Shambulio la Kigaidi..


Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa onyo kwamba magaidi huenda wakashambulia hoteli moja kubwa maarufu Jijini Nairobi ambayo hutembelewa sana Watalii na Wafanyabiashara

Taarifa ya Ubalozi huo imesema, ''Makundi ya kigaidi huenda yanapanga njama dhidi ya hoteli moja kubwa Jijini Nairobi. Hoteli inayolengwa haijatambuliwa ila inaaminika kuwa hoteli maarufu sana ya Watalii na Wafanyabiashara wa kigeni.”

Raia wa Kenya wameshauriwa kuwa waangalifu ambapo taarifa imesema, ''Unapokuwa unaishi katika hoteli tafuta njia za kutorokea. Panga mapema namna utakavyoweza kutoroka katika hoteli iwapo kutakuwa na dharura yoyote.”

Aidha, Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo, Hilary Mutyambai amewaomba Wakenya kuwa watulivu na kuwataka waendelee na shughuli zao, akisema idara ya Polisi imeimarisha usalama nchini humo pamoja na kulinda mipaka yote

Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulio kadhaa ya Kigaidi hususan karibu na mpaka wa Somalia yanayofanywa na kundi la Al-Shabaab. Itakumbukwa, Januari 15, 2019 hoteli ya Kitalii ya Dusit D2 ilivamiwa na Al-Shabaab na watu 21 waliuawa. Pia, Septemba 21, 2013 ‘Westgate Shopping Mall’ ilivamiwa na takriban watu 71 waliuawa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad