Zaidi ya Wamarekani milioni 147 waliathiriwa mwaka 2017 wakati wanaodaiwa kuwa ni wadukuzi, ambao ni wajumbe wa Jeshi la Ukombozi la Wachina (PLA), lilipoiba data mkiwemo majina na anwani
Baadhi ya wateja wa Uingereza na Canada pia waliathiriwa.
" Huu ni moja ya uingiliwaji mkubwa wa data katika ," alisema Mwanasheria Mkuu William Barr.
Equifax ilisema kuwa wadukuzi walizifikia taarifa katikati ya mwezi Mei na mwishoni mwa mwezi Julai 2017 wakati kampuni ilipogundua uingiliaji huo wa data.
Kampuni ya Equifax inatunza data za watu zaidi ya 91 milioni.
Katika taarifa yake Bwana Barr alisema: "Huu ulikua ni uingiliaji wa makusudi wa taarifa za kibinafsi za watu wa Marekani.
"Leo tunawawajibisha wadukuzi wa PLA kwa vitendo vyao vya uhalifu, na tunaikumbusha serikali ya Uchina kwamba tunauwezo wa kubaini alama zao za siri na kuwapata wadukuzi ambao taifa linawatuma mara kwa mara dhidi yetu ."
Equifax ilisema kuwa wadukuzi waliingilia taarifa zake katikati mwa mwezi Mei na mwezi Julai 2017 wakati kampuni ilipogundua uingiliaji huo.
Washukiwa wanadaiwa kuwa waliingia kwenye hifadhi 34 za takriban nchi 20 kujaribu kuficha ni wapi hasa walipo.
Naibu Mkurugenzi wa FBI David Bowdich alisema kuwa hapakuwa na ushahidi hadi sasa wa kutumiwa kwa data hizo katika wizi wa akaunti binafsi za benki au kadi za benki.
Baada ya kutambuliwa kwa mdukuzi, Equifax ililipa tozo la faini ya dola milioni $700m kwa kamati ya Shirikisho ya Biashara.
Wadhinbiti wa Marekani walidai wanasema kampuni hiyo yenye makao yake Atlanta ilishindwa kuingilia kati kuulinda mtandao wao.
Takriban dola milioni $300 zililipwa ili kumaliza tatizo la wizi wa huduma za utambulisho na gharama nyingine husika za waathiriwa.
Katika taarifa Bwana Barr alisema: "Huu ulikua ni uingiliaji wa makusudi wa taarifa za kibinafsi za watu wa Marekani.
Uchina bado haijatoa maelezo yoyote juu ya mashtaka hayo.