Masauni: Polisi haina pesa ya kufunga CCTV



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amewataka Wabunge kushirikiana na wadau mbalimbali katika maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha wanachangia upatikanaji wa CCTV Camera, zitakazofungwa katika vituo vya polisi nchini ili kuepusha malalamiko ya wananchi.

Hayo ameyabainisha leo Februari 5, 2020, Bungeni Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tauhida Gallos, lililohoji umuhimu wa kufunga CCTV Camera katika vituo vya polisi, zitakazomuwezesha Mkuu wa Kituo kufuatilia na kujua ni nini kinachoendelea kituoni.

"Jeshi la Polisi halina bajeti ya kuwezesha ufungaji wa CCTV Camera vituoni, hivyo Wabunge mshirikiane na wadau ili Camera hizo zinunuliwe zifungwe na kupunguza malalamiko ya huduma isiyo na weledi ya askari kwa wananchi" amesema Mhandisi Masauni.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad